Picha ya maktaba/ MTANDA BLOG
Juma Mtanda, Morogoro
Morogoro: Watoto wawili wa shule za
msingi Ifakara na Mbasa wilaya ya Kilombro, Mkoani Morogoro wamefariki dunia
baada ya kusombwa na maji ya mafuriko wakati wakiogelea katika mfereji
unaopokea maji kutoka mto Lumemo baada ya mvua kubwa kunyesha.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti
hili katika mji wa Ifakara, Afisa Mtendaji wa kata ya Viwanja Sitini, Gregory
Midas alisema kuwa watoto hao wamefariki dunia April15 mwaka huu majira ya saa
3 asubuhi wakati wakiogelea katika mfereji huo.
Aliwataja wanafunzi hao kuwa
ni, Ester Kong’oa (13) anayesoma darasa la sita katika shule ya msingi Ifakara
na, Rehema Lyakalyaka (12) darasa la nne katika shule ya msingi Mbasa .
Midas alisema kuwa wanafunzi
hao walisombwa na maji ya mfereji unaopokea maji kutoka kwenye mto Lumemo unaoingiza
maji katika mto Kilombero.
Midas anasema mafuriko hayo
yamesababisha shule nne kufungwa ikiwemo shule ya Sekondari Kwashungu na tatu
za msingi Ifakara, Lumemo na Mautanga.
“Hawa watoto wamekumbwa na tukio
hili baada ya kutoka shule na kwenda kuogelea kwenye mfereji unaopokea maji
kutoka mto Lumemo ambao uliofurika maji baada ya mvua kubwa kunyesha na
kusababisha maji kusambaa sehemu mbalimbal za mji wa ifakara,”alisema Mtendaji
huyo.
Midas amewataka wazazi wanaoishi
katika eneo hilo kuwa makini na watoto wao katika kipindi chote hasa kipindi hiki
cha masika.
Akiongea na gazeti hili, Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo la vifo
hivyo.
0 comments:
Post a Comment