BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAFUNZI WA CHEKECHEA ASOMBWA NA MAJI YA MAFURIKO MTONI MOROGORO

Juma Mtanda, Morogoro.
Mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Dala kata ya Mvuha, Erick Makale (6) amefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mafuriko wakati akiongelea na wenzake katika mto Mvuha majira ya saa 10 jioni April 23 mwaka huu, Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa kijiji cha Dala, Boi Lubegete alisema kuwa Erick amefariki dunia kwa kusombwa na maji ya mafuriko na mwili wake bado haujaonekana.

Lubegete alisema kuwa marehemu alikuwa na wenzake watatu na waliingia kuogelea mtoni baada ya kumaliza kazi ya kufua nguo lakini yeye aliingia kwenye kina kirefu kisha maji kumsomba tofauti na wenzake waliokuwa kwenye kina kifupi.

“Watoto wenzake walieleza kuwa baada ya Erick kuzidiwa nguvu kisha kusombwa na maji hayo aliweza kushika mti kando ya mto huo lakini baadaye aliuachia na kuzama na mpaka leo bado mwili wake haujapatikana”.alisema Lubegete.

Wakati huo huo Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini imetoa msaada wa vyakula kwa kaya 86 zilizokumbwa na mafuriko wenye thamani ya sh3.5Milioni kata za Selembara na Mvuha mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Erinest Khisombi alisema kuwa serikali ya wilaya imetoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo baada ya kamati ya ulinzi na usalama kutembelea maeneo husika.

Khisombi alisema kuwa msaada huo umekuja baada ya wakazi wa kata hizo kukosa makazi kutokana na kubomoka kwa nyumba, vyakula na mazao kusombwa na maji.

“Tumetoa msaada wa mifuko 100 za kg 25 za unga wa mahindi, maharage kg 200 na mafuta ya kupikia lita 100 vyote vikiwa na thamani ya sh3.5Mil ikiwa ni hatua yetu ya dharura kwa wahanga hao ili iweze kuwasaidia”.alisema Khisombi.

Aliongeza kwa kusema kuwa mafuriko hayo yamesababisha hasara kubwa kwa wananchi waliokumbwa na mkasa huo.chanzo/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: