BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DKT JOHN MAGUFULI ANAKUMBUSHA ENZI ZA EDWARD MORINGE SOKOINE.


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya kwanza, Edward Moringe Sokoine.

Dar es Salaam.
Vita aliyoianzisha Rais John Magufuli ya kupambana na rushwa, ufisadi na uzembe kazini, inaibua kumbukumbu muhimu hasa leo; inakumbusha utendaji wa Edward Sokoine, mmoja wa mawaziri wakuu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Leo ni siku ya kukumbuka kifo cha Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa mkoani Morogoro wakati akitokea bungeni mjini Dodoma kwenda Dar es Salaam, ajali iliyoacha maswali mengi kutokana na ulinzi anaokuwa nao mtendaji mkuu wa Serikali.

Likiwa katikati ya msafara, gari alilopanda Sokoine liligongwa na gari jingine aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na Dumisani Dube, raia wa Afrika Kusini ambaye baadaye alifungwa jela na alipotoka alirejeshwa kwao.

Sokoine alikufa wakati akiwa katikati ya vita dhidi ya wahujumu uchumi, wala rushwa, mafisadi na wazembe kazini, ambayo ilisababisha wafanyabiashara wengi kukimbia nchi, kutelekeza mali zao huku watendaji wa Serikali wakiachishwa kazi.

Matukio kama hayo yametawala wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajaribu kujenga nidhamu ya uwajibikaji, kudhibiti matumizi ya umma, wizi, ukwepaji kodi na uzembe kazini.

bungeni mjini Dodoma kwenda Dar es Salaam, ajali iliyoacha maswali mengi kutokana na ulinzi anaokuwa nao mtendaji mkuu wa Serikali.

Likiwa katikati ya msafara, gari alilopanda Sokoine liligongwa na gari jingine aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na Dumisani Dube, raia wa Afrika Kusini ambaye baadaye alifungwa jela na alipotoka alirejeshwa kwao.

Sokoine alikufa wakati akiwa katikati ya vita dhidi ya wahujumu uchumi, wala rushwa, mafisadi na wazembe kazini, ambayo ilisababisha wafanyabiashara wengi kukimbia nchi, kutelekeza mali zao huku watendaji wa Serikali wakiachishwa kazi.

Matukio kama hayo yametawala wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajaribu kujenga nidhamu ya uwajibikaji, kudhibiti matumizi ya umma, wizi, ukwepaji kodi na uzembe kazini.

Wakizungumza na Mwananchi kuhusu kumbukumbu ya Sokoine, wanafamilia, wanasiasa na wadau wengine walimfananisha Magufuli na waziri huyo mkuu ambaye taswira yake inahusishwa na vita dhidi ya uhujumu uchumi.

“Sokoine alikuwa hapendi ubadhirifu kama alivyo Rais Magufuli, na vilevile ni miongoni mwa viongozi waliochukia sana ufisadi,” anasema mwanasiasa mstaafu, Chrisant Mzindakaya ambaye alijijenge umaarufu kama “mzee wa mabomu” kutokana na kuibua bungeni kashfa zilizosababisha mawaziri wawili waachishwe kazi.

“Kama unakumbuka mwaka ule (aliofariki) ndio tulifanya kampeni ya uhujumu uchumi mimi nikiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

“Kwa hiyo mambo yanayofanyika sasa ya kupiga vita ubadhirifu na kupiga vita ufisadi yalianza wakati ule na alisimamia kwa dhati ya moyo wake.”

Moses Sokoine, kaka yake Sokoine, anafananisha hatua ambazo Rais Magufuli anachukua hivi sasa na vita ambayo aliianzisha mdogo wake. “Ninaposikia mambo ambayo anafanya sasa Rais Magufuli, naona kama alivyokuwa mdogo wangu,” alisema alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kijijini kwao Monduli Juu.

“ Watanzania tumuombee kwa kuwa kazi anayofanya ni ngumu na inampa maadui kama ilivyokuwa kwa Sokoine.”

Moses anasema tangu kifo chake, ilikuwa ngumu kumpata mrithi wake hasa katika vita dhidi ya rushwa, uhujumu uchumi, magendo, uwajibikaji na ubadhilifu wa mali za umma.

Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Bora ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Elijah Kondi alisema kwa kigezo cha muktadha inakuwa vigumu kulinganisha utendaji wao, lakini kwa tabia na haiba ya uchapakazi wanashabihiana kwa kiasi kikubwa.

Kondi alisema Hayati Sokoine alikuwa kiongozi asiyependa uvivu, uzembe na alikuwa mkweli na mfuatiliaji wa taarifa za watendaji wake, hali inayoonekana wazi kwa Rais Magufuli. 


“Kwa mazingira hayo wanaonekana kuwa sawa, tunaweza kumkumbuka kwa nafasi hiyo. Kwa mfano hata uamuzi alioufanya leo (jana wa kutengua uteuzi wa Anne Kilango kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), ni wazi kwamba, alipokea taarifa na ameamua kuzifanya kazi. Ni sawa na tabia ya Sokoine,” alisema.

Profesa George Shumbusho kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema aliyemfahamu Hayati Sokoine atamuona wazi kwa Rais Magufuli kupitia ishara mbalimbali na maamuzi anayochukua.

Profesa Shumbusho alisema kila alichokisema Hayati Sokoine alimaanisha usoni kwake, sawa na Rais Magufuli.

“Enzi hizo, mtumishi wa umma akisikia (Sokoine) anamtembelea ofisini kwake, lazima atakuwa na hofu sawa na ya kutumbuliwa,” alisema Profesa Shumbuso.

“Hakuwa kiongozi wa kupepesa macho na alipenda kutetea wanyonge.”MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: