Maji yenye vimelea vya kisonono kutoka mwilini mwa binadamu, kama inavyoonekana kwenye darubini.
Madaktari wameelezea hofu yao kutokana na usugu wa maradhi ya kisonono cha aina mpya, kilichogundulika nchini hapa na kusambaa kwa kasi kubwa.
Kwa mujibu wa madaktari hao, aina hiyo ya kisonono kilichopewa jina la 'Super Gonorrhea' kimeathiri pia kundi la mashoga na jamii yote inayofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mwaka jana, kulipuka kwa maradhi hayo ambayo mgonjwa wa kwanza aligundulika huko Leeds, sasa idadi ya wagonjwa imeongezeka na kufikia 34, huku madaktari wakidai juhudi zao za matibabu zinaonyesha dalili za kukwama.
Idara ya Afya ya Uingereza, imesema kuwa iwapo hatua za uhakika hazitachukuliwa, kuna hatari maradhi hayo yatashindikana kutibiwa. Njia kuu ya kusambaa kwake ni tendo la mapenzi.
Hivi sasa kuna wagonjwa wa kisonono cha aina hicho wanaopatikana katika baadhi ya maeneo kama vile Kusini mwa Uingereza, Midlands na jijini London.
Wakati inaelezwa kwamba wagonjwa wa kwanza walionekana kuwa 'bibi na bwana' hivi sasa hali inakuwa mbaya kwa mashoga nao ni waathirika ndani ya kipindi kifupi.
Msemaji wa Idara hiyo ya afya, Peter Greenhouse, anasema hiyo ni ishara kwamba kasi ya watu kufanya ngono ni kubwa.
Anataja ishara ya mtu kuwa na kisonono ni mgonjwa kutoa maji kijani au njano katika sehemu ya siri, inayoendana na maumivu makali wakati wa kupata haja ndogo na hedhi kwa kinamama.
Hatari nyingine ya kisonono inaweza kuzuia uzazi kwa mwanamke na ugonjwa kumuambukiza mtoto, iwapo anayeugua ni mjamzito.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment