Mkuu wa Masoko
na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita
Makamba (katikati) akigonganisha chupa za shampeini na warembo.Picha ya maktaba.
Utafiti umebaini kwamba asilimia 71 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wanatumia muda wao mwingi kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali.
Badala yake hutumia muda huo kujihudumia kwenye gesti, baa, kulala na katika shughuli za starehe.
Serikali imesema hali hii inaichelewesha Tanzania kuingia katika kundi la mataifa yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Bi Ruth Minja, ambaye ni mtakwimu mkuu katika ofisi ya taifa ya takwimu Tanzania, ndiye aliyeongoza utafiti huo wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka 2014/2015.
Anasema waligundua kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa milioni 25 kutokana na kiashiria cha saa za kufanya kazi kupungua na baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa kazi kutokana na utendaji dhaifu.
Ally Msaki, aliyemuwakilisha katibu mkuu katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu amewaangazia Watanzania walioko kwenye ajira, ambao wanapata kipato ambacho hakitoshelezi kuweza kumudu gharama za maisha.
Amesema nafasi kama hizo za kazi hazina viwango vya ubora na ni kinyume cha maelekezo ya shirika la wafanya kazi duniani ILO.
Ingawa Sera ya taifa ya ajira kwa Taifa la Tanzania kwa mwaka 2008 ilijikita zaidi katika kuongeza fursa za ajira na kufanikiwa katika lengo lake, kuna kasoro kwenye kipengele cha ubora wa ajira.
Magufuli: Vijana sharti wafanye kazi
Rais wa Tanzania John Magufuli amelalamikia tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni na kucheza pool badala ya kufanya kazi mijini na maeneo ya mashambani.
Rais Magufuli ametoa wito kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha watu wanafanya kazi hususani vijana.
"Haiwezekani vijana wawe wanashinda vijiweni wanacheza pool, wakati wazee na akina mama wapo mashambani wanalima. Kawahimizeni wafanye kazi, wasipofanya kwa hiari walazimisheni kufanya kazi," amesema Rais Magufuli, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Kiongozi huyo alitoa agizo hilo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa 25 pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jumanne.
Dkt Magufuli amewataka kwenda kufanya kazi kwa kujiamini na kujielekeza kutatua kero za wananchi.
Amewataka wakuu hao wa mikoa kusimamia ulinzi na usalama katika mikoa yao.
Aidha, Dkt Magufuli amewaagiza kusimamia udhibiti wa fedha za umma katika halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji na kumetoa siku 15 kwa halmashauri hizo pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali kuondoa majina ya wafanyakazi hewa katika orodha za mishahara ya watumishi wa umma.
Dkt Magufuli amewasisitiza wakuu hao wa Mikoa kutosita kufanya maamuzi na kuchukua hatua haraka, huku akitaka wawasimamie ipasavyo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu wa tarafa na watendaji wa kata na vijiji ili watekeleze wajibu wao.BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment