BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMKE AFUKUZWA KAZI KWA SABABU YA KUKATAA KUVAA VIATU VYENYE VISIGINO VIREFU

Karani mmoja wa kupokea wageni mjini London alilazimika kurudi nyumbani baada ya kukataa kuvaa viatu vyenye visigino virefu,imebainika.

Mfanyikazi huyo wa kampuni ya Temp, Nicola Thorp mwenye umri wa miaka 27 kutoka Hackney aliwasili katika kampuni moja inayoshughulikia maswala ya kifedha PwC kabla ya kuarifiwa kwamba anahitajika kuvaa viatu vyenye visigino vya nchi 2 hadi 4.

Alipokataa na kulalamika kwamba mbona wenzake wa kiume hawakutakiwa kuvaa hivyo,alitakiwa kurudi bila ya mshahara.

Kampuni ya Portico imesema kuwa iliweka sheria hizo kwa wafanyikazi wanaokabidhiwa PwC lakini imesema kuwa haitaondoa sheria hiyo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: