BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEZEA SERIKALI NINI !!! WALIMU WALIPWA VIFARANGA VYA KUKU KAMA SEHEMU YA PESA ZA MSHAHARA WA MWEZI.


Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa. 


Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakitia vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo.

Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani{Radio Ozodlik} kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka.

Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni, lakini wanataka pesa zao.

Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni.

Mamlaka za Uzbekistan hazikubalii uhuru wa vyombo vya habari na raia wa huko hutegemea vyombo vya habari vya kimataifa kutoa sauti yao, ila hawajitambulishi.

Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni.

Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: