BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATUMISHI HEWA 11 WATAFUNA KIASI CHA SH Sh57.7 MIL NAMNYUMBU



Nanyumbu. Halmashauri ya wilaya Nanyumbu imebaini watumishi 11 zaidi hewa ambao wamesababisha hasara kiasi ya Sh57,756,984.20 baada ya uhakiki.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu, Idris Mtandi Katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbu kinachoendelea sasa.

Idris Mtandi amesema watumishi hewa wote wamebainika kuwa ni walimu wa shule za msingi na sekondari ambao wamekuwa wakipokea mishahara bila kufanya kazi.

Amesema changamoto kubwa ni namna taratibu za nidhamu zinavyotakiwa kuwa kwa kuwa mamlaka ya nidhamu ya walimu TSD inavyochelewa kutoa maamuzi ya kinidhamu kwa walimu. 


Hata hivyo, amesema mamlaka ya nidhamu ya walimu sasa itarudishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji ili aweze kuchukua hatua haraka kuliko ilivyo sasa.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: