DIAMOND APIGIWA MAKOFI BUNGENI NA WABUNGE DODOMA
Kutoka kushoto, Nhlanhla Nciza wa kundi la Mafikizolo-Afrika kusini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba, Naseeb Abdul Juma “Diamond Platnumz”, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Theo Kgosinkwe wa kundi la Mafikizolo
Dodoma. Mwanamuziki Nasib Abdul maarufu kama Dimond
ameibua hisia za wabunge bungeni wakati akitambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kumshangilia kwa makofi na vigelegele.
Akitambulisha wageni waliofika bungeni, Ndugai alisema Diamond aliongozana na wanamziki wenzake kutoka Afrika Kusini wanaojulikana kama Mafikizolo.
Ndugai alisema wanamuziki hao ni wageni wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
Alisema, “wanamuziki hawa wa Mafikizolo wameongozana na mwenyeji wao kijana wetu anayeitangaza nchi huko duniani, Nasib Abdul au Diamond,” alisema Spika na kuwafanya wabunge kulipuka kwa makofi na vigelegele.
Hali hiyo iliwafanya wabunge kuangalia katika ukumbi wa wageni uliomo ndani ya Bunge ambao walikuwa wamekaa wageni hao huku Diamond akishukuru kwa kuinama kwa zaidi ya mara tatu.
“Ujio huu wa Diamond unatoa hamasa kwamba kuna kitu leo jioni kinafanyika, tunaomba waziri wa habari atutaarifu ili tujumuike pamoja,” alisema.
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha asubuhi, Ndugai amesema amepokea taarifa kutoka kwa Nape kwamba Diamond atumbuiza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akiwa na Mafikizolo.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment