AHUKUMIWA KWA KUTEMBEA KWA MIGUU UMBALI MREFU.
Mwanamame mmoja raia wa Sudan amehukumiwa kifungo cha miezi tisa jela na mahakama moja nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kutembea kwa miguuu kutoka nchini Ufaransa hadi Uingereza akipitia njia ya reli.
Raia huyo aliyetambulika kwa jina la, Abdul Rahman Haroun mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikiri mashtaka hayo alikuwa amepewa hifadhi nchini Uingereza mwaka uliopita.
Haroun anaaminika kutembea umbali wa kilomita 50 kutoka Calaisin nchini Ufaransa, hadi Folkestone nchini Uingereza kabla ya kupatikana tarehe 4 mwezi Agosti mwaka jana.
Hata hivyo Haroun hawezi kufungwa jela kutoka na kipindi kirefu ambacho tayari amekuwa kizuizini kinatosha kuwa adhabu ya kosa hilo.
0 comments:
Post a Comment