BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HEKIMA NA BUSARA ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA.

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema watu watakaopanda pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (Helmet) watakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kutaka kujaribu kujiua. 

MTANDA BLOG inaungana na kauri ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa amri aliyoitoa kwa madereva pikipiki maarufu kama (Bodaboda) Tuna amini itasaidia madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani pengine na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

"Si vibaya na mikoa mingine kujaribu kubuni mbinu zitakazosaidia kuwalazimisha waendesha pikipiki kutii sheria bila shuruti kwa kuweka vikwazo vya kisheria vyenye lengo la kuwasaidia watii sheria kwa kuhofia kukumbwa na adhabu kali".

Moja ya makosa ya makusudi yanayofanywa na waendesha pikipiki ni pamoja na kuzibua bomba la kutolea hewa chafu (Eksosi) na n:k unaofanya utoe mlio kama pikipiki za mashindano na kusababisha kero nyakati za usiku wakati wakiendelea na biashara zao za kubeba abiria.

Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment