
Msanii mashuhuri wa filamu nchini Marekani, Will Smith na aliyekuwa bingwa wa dunia wa uzani wa juu Lennox Lewis, wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu watakaobeba jeneza la bondia bingwa mara tatu duniani marehemu Muhammed Ali.
Mwaka wa 2001 Smith aliigiza katika filamu kumhusu Muhammad Ali kama Ali, jambo lilimsababisha kuteuliwa katika tuzo la Oscar.
Tangu hapo amekuwa rafiki wa familia hiyo ya Muhammad Ali.
Lewis kwa upande wake ni miongoni mwa mabondia watatu kwa pamoja na Ali na Evander Holyfeild ambao wamewahishinda taji la uzani wa juu mara tatu.

Wawili hao sasa wataungana na jamaa na marafiki kuubeba jeneza la Ali, mjini Kentucky siku ya Ijumaa wakati wa mazishi yake.
Ali alifariki siku ya Ijumaa mjini Arizona alikokuwa amelazwa hospitalini akiwa na umri wa miaka 74.

MOHAMMED ALI KUZIKWA IJUMAA MAREKANI
Mwili wa Muhammad Ali umewasili katika mji wake wa Louisville, Kentucky ambapo mazishi yake yatafanyika siku ya Ijumaa.
Jeneza la nguli huyo wa masumbwi nchini Marekani ulisafirishwa katika msafara wa magari uliotokea katika uwanja wa ndege wa Louisville mpaka katikati ya mji.
Ali ni miongoni mwa wanamichezo mashuhuri waliofanya vizuri katika karne ya ishirini na salamu za rambi rambi zinaendelea kumiminika kutoka shehemu mbalimbali baada ya kifo chake kilichotokea siku ya Ijumaa.
Mazishi yake yanatarajiwa kuwa makubwa.

0 comments:
Post a Comment