BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IKIWA ZIMEBAKIA SIKU 9 KUZIMWA KWA SIMU FEKI HIZI NDIZO HATUA ZA KUCHUKUA MTUMIAJI.

Juni 16, 2016 simu feki zitazimwa.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Juni 16, 2016 inatarajia kuzima simu zote feki nchini. 

Hii ni kufuatiwa taarifa iliyotolewa na wataalamu wa mamlaka hiyo kuwa simu hizo zina madhara makubwa sana kwa watumiaji wake kwa sababu zipo chini ya viwango vinavyotakiwa.

Kumekuwa na watu wengi wakijiuliza kama simu zao nao zitazimwa au la kwa sababu hawana uhakika kama nazo ni miongoni mwa simu feki au la. 

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania imetoka utaratibu ambao kila mmoja anaweza kuangalia kama simu yake/zake ni feki au original.

Namna ya kuhakiki IMEI ya simu yako kujua kama ni feki au sio feki.

Piga *#06# kwenye simu yako ya mkononi na namba itakayoonekana kwenye simu yako inaitwa IMEI na haifanani na ya simu nyingine yoyote ile. 

Kwa simu zenye kadi za simu mbili (laini mbili) simu yako itaonyesha IMEI mbili.

Kisha tembelea bofya link hii http://www.tcra.go.tz/index.php/imei-code-verification na namba iliyojitokeza baada ya kupika *#06# utatakiwa kuiingiza kwenye sanduku (box) lililowazi kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa “verify my device”. 

Baada ya kubonyeza, kampuni iliyotengeneza simu yako, itaoneex ex eskana hapo kutokana na namba itakayokuwa umeinginza na itakuonyesha kama simu yako ni feki au sio feki.

Kama simu yako ni feki, chukua tahadhari mapema kwani ni siku tisa tu ndizo zimesalia kabla simu hizo hazijazimwa. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: