BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAISHA YA BONDIA MASHUHURI MUHAMMAD ALI KATIKA MATUKIO YA PICHA ENZI ZAKE ZA UHAI

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha zinazosimulia matukio muhimu katika maisha ya Muhammad Ali, bingwa wa ndondi na mwanamichezo mashuhuri.
Ali alijaribu kupigania taji la ubingwa duniani februari 1964 alipokabiliana na bingwa wa dunia Sonny Liston. Liston alisema: "Nafikiri nitampiga vibaya sana kijana huyo."
Alidunishwa na wataalamu wengi wa masumbwi kabla ya pambano hilo lakini Ali alicheza kwa ustadi mkubwa Miami na kumlazimisha Liston kusalimu amri kabla ya raundi ya sita. Ali alitawazwa bingwa wa dunia uzani wa heavyweight akiwa na umri wa miaka 22.

Ushindi wa Ali dhidi ya Liston ulikuwa, na bado ni, moja ya matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya ndondi. Ali alijisifu: "Mimi ndiye bingwa zaidi! Mimi ndiye bora zaidi! Mimi ni mfalme wa dunia!".
Ali, alitangaza kujiunga na kundi la Nation of Islam na akaacha kutumia majina yake ya awali na kuwa Muhammad Ali baada ya pambano hilo dhidi ya Liston. Alitetea ubingwa wake dhidi ya Liston mjini Lewiston, Maine mwezi mei 1965.
Ali alishinda Liston baada ya kumpiga knock-out dakika ya kwanza ya raundi ya kwanza. Hadi wa leo, wengi wanaamini Liston aliuza pambano hilo, lakini Ali amesisitiza kwamba alishinda kwa njia safi.
Novemba 1965, Ali alitetea taji lake dhidi ya bingwa wa zamani Floyd Patterson akishinda kwenye raundi ya 12. Patterson alikuwa amemshambulia sana Ali kuhusu msimamo wake kisiasa na kidini.
Ali alirejea London kupigana na Henry Cooper kwa mara ya pili Mei 1966 katika uwanja wa zamani wa Arsenal wa Highbury. Mashabikji wake Uingereza, ambao hawakuwa wamemtambua mara ya kwanza, walimshabikia sana. Angelo Dundee, anayeonekana hapa akifunga mikono ya Ali kabla yake kupambana na Cooper, alikuwa akimsaidia Ali tangu alipoanza kucheza ndondi. "Kuna Cassius Clay mmoja," alisema Dundee. "Namshukuru Mungu."
Muhammad Ali Ali alimshinda Cooper baada ya raundi sita na kumuumiza vibaya karibu na jicho lake la kushoto. Baada ya kifo cha Cooper 2011, Ali alisema: "Nitamkosa sana rafikin yangu wa zamani - alikuwa mpiganaji hodari na mwanamume muungwana."
Ali alitetea taji lake mara ya nane dhidi ya Ernie Terell Februari 1967. Ali alimchezea Terrel ambaye alikuwa ametumia jina lake la kuzaliwa kumrejelea yeye kabla ya mechi, kwa raundi 15. Kila mara alikuwa akimwuliza: "Jina langu ni nani, Mjomba Tom?"


Baada ya kutetea taji lake tena mara nyingine dhidi ya Zora Folley, Ali alipokonywa taji lake baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lililokuwa likipigana vita Vietnam. Ilikuwa ni miaka mitatu baadaye aliporejea ulingoni tena. Ali alishinda marudio ya pambano hilo dhidi ya Frazier ingawa pambano lake linalosifika sana lilijiri baadaye 1974 alipopigana na George Foreman katika pambano linalojulikana kama "Rumble in the Jungle" maana yake "Mngurumo Msituni". Ali alikaa raundi nane za kwanza akiwa amejibanza kwenye kamba, mbinu aliyoiita 'rope-a-dope'.Lakini alichomoka raundi ya nane na kumwangusha Foreman kwa ngumi kali na kuwa mwanamume wa pili kutwaa tena ubingwa wa heavyweight, akiwa na umri wa miaka 32.
Ali alipoteza taji lake kwa Leon Spinks 1978 kabla ya kulitwaa tena kwa mara ya tatu baadaye mwaka huo. Alitangaza kustaafu kwake miezi tisa baadaye. Lakini alirejea 1980 na kupigana na bingwa mpya Larry Holmes.
Baada ya kushindwa na Holmes, Ali alipigana pambano moja, dhidi ya Trevor Berbick ambapo alishindwa kabla ya kustaafu kabisa akiwa na umri wa miaka 40. Kuondoka kwake kuliacha pengo katika tasnia ya ndondi, lililojazwa tu na kufika kwa Mike Tyson katikati mwa miaka ya 1980.
Ali aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa Parkinson (ugonjwa wa kutetemeka) mwaka 1984 lakini alikabiliana na hali hiyo kwa ujasiri na staha. Mwaka 1996, alitazamwa na mabilioni ya watu akiwasha mwenye wa Olimpiki mjini Atlanta.Atlanta pia, alipewa tena nishani yake ya dhahabu kutoka kwa Michezo ya Olimpiki ya 1960. Ali alidai aliirusha nishani yake ya kwanza Mto Ohio baada ya kukosa kuhudumiwa katika mgahawa wa Wazungu pekee, ingawa wengi hutilia shaka hilo.Wakati wa kufunga karne, Ali alijizolea sifa tele. Watazamaji wa BBC walimpigia kura kuwa Mchezaji Bora zaidi wa Karne, mwaka ambao bondia wa Uingereza Lennoz Lewis alishinda tuzo kuu.Bintiye Ali, laila alianza kucheza ndondi akwia na umri wa miaka 15 na akaanza kucheza ndondi ya kulipwa 1999 kabla ya kumshinda bintiye Frazier, jackie Frazier-Lyde mwaka 2001. Laila alishinda taji la super-middleweight mwaka 2002 kabla ya kustaafu 2007.Mwaka 2001, filamu kuhusu maisha ya Ali ilitolewa, Ali akiigizwa na Will Smith. Ali aliendelea kusifika kote duniani, licha ya afya yake kudorora.Baada ya kutimiza umri wa miaka 70, afya yake ilidhoofika zaidi. "Nafikiri kuugua kwangu ugonjwa wa Parkinson ni njia ya Mungu kunikumbusha ni nini cha muhimu zaidi," ndivyo alivyosema. Amefariki akiwa na umri wa miaka 74.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: