IRENE KOMBA.
Mfano
kodi ya vat ya 10% ya utumaji wa fedha katika simu kwenda kwa mpokeaji
inaumiza pande zote mbili ila mtu wa mwisho ndiye anayeumia zaidi.
Ikipitishwa hiyo bajeti mtu wa kijijini ndiye atayeumia zaidi kwani atalazimika makampuni ya simu kumkata zaidi ya asilimia 10 maana katika kupokea fedha kutoka mtumaji atakatwa asilimia na wakati wa kutoa fedha hizo atakatwa tena asilimia, naona serikali imekuja katika kumkandamiza mwananchi wa kawaida tu.

BONINVETURE MTALIMBO.
Nimevutiwa na bajeti ya mwaka 2016/2017 ya kuwata wabunge kuwa sehemu ya viongozi wa Tanzania kuwajibika katika kulipa kodi kwani wao ni sehemu ya wananchi na kuwa wanapaswa kuonyesha mfano kwa wananchi katika uwajibikaji wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.
MDINI MOHAMED MSUMI (46).
Bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha na mipango hasa sekta ya fedha iendeleza kuwaminya kiuchumi wananchi wa kawaida hali itayopelekea kuongezeka ugumu wa maisha badala ya kupunguza makali ya maisha yaliyo sahihi.
Bajeti ya mwaka 2016/2017 ya 9% ambayo serikali imepunguza kutoka asilimia 11 ambayo mfanyakazi analipa malipo yake (P.A.YE) haimsaidii mlengwa.
Kwa
sababu 9% ni fedha ndogo sana ukilinganisha ongezeko la fedha katika
mshahara kwani mahitaji halisi ya maisha bado inamuumiza mfanyakazi, imeandaliwaa na MTANDA BLOG.

0 comments:
Post a Comment