Aliwahi kuulizwa malakal maut na ALLAH S.W Jee uliwahi kulia au kucheka pindi unapotoa roho za waja wangu ?.Akajibu niliwahi kulia, kucheka na kupatwa na fazaa.
Nilicheka siku moja nilipokwenda kwa mtu mmoja kuchukuwa roho yake nikamkuta anaongea na fundi wa viatu akimuambia nishonee vizuri nivae mwaka mzima, nitanunua vipya mwakani nikacheka na kuichukuwa roho yake kabla hajavivaa.
Na kilichoniliza ni siku Ulinituma kuchukuwa roho ya mwanamke mmoja aliekuwa pangoni peke yake akimnyonyesha mwanawe na hakuna mtu aliekuwa anajua mahali alipo basi nikaitoa roho yake huku mtoto akilia kwa uchungu na mimi nikalia.
Na kilichonipa fazaa ni siku ulionituma nikachukuwe roho ya mcha Mungu sana wakati nilipoingia chumbani mwake nikakuta chumba chake kimegubikwa na nuru nikapata tabu kumfikia nilipokuwa natoa roho yake fazaa kubwa ikanishika.
ALLAH S.W akamuuliza jee unamfahamu mtu huyo?
Akajibu malakal maut: lah simfahamu zaidi ya kuwa ni mwanachuoni.
ALLAH S.W akamuambia huyo ni yule mtoto aliyekuwa akinyonyeshwa na mama yake pangoni na ukaichukuwa roho ya mama yake
Huyo ndio malakal maut anaewatenganisha wapendanao mama na mtoto wake, mtu na mkewe, mtu na rafiki yake mtu na mzazi wake.
Basi usimsahau malaika huyu hakika yeye hakusahau inapokuja amri kwake kaniitie mja wangu fulani basi hushuka kwa haraka na kutii amri ya ALLAH S.W tukumbuke ipo siku na saa atatutembelea wakati wowote saa yoyote dakika yoyote sekunde yoyote.
Tukae tukilitaffakar hili kwani huenda chochote kile tunachokifanya kikawa ndio tendo letu la mwisho au ikawa ndio kauli ya mwisho.
Tumuombe ALLAH S.W atupe khatma njema katika matendo yetu ya mwisho na atujaalie kauli yetu ya mwisho iwe LAAILAHA ILLA LLAH MUHAMMADU RASSULU-LLAH
AMIN.
FADHAKIR FAINNA DHIKRA TANFAUL MUUMININ.

0 comments:
Post a Comment