BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MIHOGO YAUA WATU WATATU MOROGORO



Juma Mtanda, Morogoro
Watu watano wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti huku wengine wakinusuriki kifo baada ya kudaiwa kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kamanda wa polisi mkoa wa, Ulrich Matei alisema kuwa matukio hayo yametokea katika vijiji vya Kikeo wilaya ya Mvomero na Kauzeni Manispaa ya Morogoro.

Matei alisema kuwa katika tukio lililotokea Juni 18 majira ya saa 9 mchana eneo la kijiji cha Kauzeni kata ya Mzinga Manispaa ya Morogoro watu watano wanadaiwa kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu, watatu walifariki dunia na wengine wawili wamenusurika vifo.


“Jana (juzi) watu watatu wamefariki dunia baada ya kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu ambapo mmoja alifariki dunia eneo la tukio akifahamika kwa jina la Daudi Hermani (31) na wengine wanne kukimbizwa hospitali ya jeshi Mzinga Manispaa ya Morogoro.”alisema Matei.

Waliokimbizwa hospitalini hapo ni pamoja na Amosi Kunambi (30), Omary Mohamed (35), Hamis Mohamed (35) na Joshua Msiani (28).
Kamanda wa polisi mkoa wa, Ulrich Matei

Kamanda Matei alisema kuwa baada ya hali zao kuwa mbaya mara baada ya kufikishwa hospitali ya Mzinga, hali za wagonjwa hao zilibadilika hafla na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo wawili kati yao walifariki dunia akiwemo, Omary Mohamed (35) na Hamis Mohamed (35) ambao ni mapacha.

Hata hivyo, Amosi Kunambi alitibiwa katika hospitali ya rufaa kisha kupata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani huku Joshua Msiani akiendelea kupatatiwa matibabu hospitalini hapo wakatii miili ya marehemu ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa.

 
Mihogo ikiwa imetayarishwa tayari kwa mlo wa chakula.

Katika tukio lingine mkazi wa kijiji cha Kikeo tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero, Jackson John (25) anadaiwa kuchukua mkuki na kumchoma mdogo wake eneo la tumbo, Raymond Melikioni (9) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kikeo na kufariki dunia papo hapo.

Kamanda Matei alisema kuwa, Jackson John anasadikiwa kuwa na ugonjwa wa akili na mara baada ya kutenda tukio hilo ndipo na yeye kuchukua jukumu la kujichoma na mkuki huo huo eneo la ubavuni katika mwili wake na kufariki dunia.

“Matukio hayo yote jeshi la polisi yanayafanyia uchunguzi ili kubainini vyanzo vyake na hili la vifo vinavyohusisha ulaji wa mihongo uchunguzi wa kitabibu unaendele ili kuona kama kweli mihogo hiyo ilikuwa na sumu.".alisema Kamanda Matei.


Tayari sampuni imechukuliwa na kupeleka kwa mkemia mkuu wa serikali na tutatoa ripoti baada ya kutoka majibu.”alisema Kamanda Matei.CHANZO:MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: