BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENGE WA UHURU WATUA MBEYA, KUFUNGUA MIRADI 59 YA SH12 BILIONI

UJUMBE WA MBIO ZA MWENGE MWAKA HUU NI VIJANA NGUVU KAZI YA TAIFA WASHIRIKISHWE NA KUWEZESHWA.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa mkoani humu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla Leo amepokea Mwenge wa Uhuru toka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh.Rehema Nchimbi.
Mwenge wa Uhuru umepokewa Leo tarehe 24 Juni 2016, Mkoani Mbeya kutoka Mkoa wa Iringa. 


Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Mbeya utakimbizwa kwa umbali wa Kilomita 1,321.8,katika wilaya 5 na Halmashauri 7 za Mkoa wa Mbeya hadi tarehe 01 Julai 2016 utakapokabidhiwa Mkoa wa Songwe. 
 
Akizungumza na wananchi Mh.Rc Makalla akitoa taarifa ya Mkoa Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Joh P.Magufuli kuhusu mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Mbeya ,amesema utatembelea Miradi 59 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 12 Kati ya Miradi hiyo Mwenge wa Uhuru utazindua/kufungua Miradi 34 , kuweka mawe ya msingi miradi 10 na kukagua miradi 15.

Kati ya fedha hizo, fedha za serikali kuu ni Sh.1,704,408,701.00 ,fedha za Halmashauri ni Sh. 1,044,682,346.00 ,Nguvu za wananchi ni Sh. 7,297,995,162.00 ,Fedha za wahisani ni Sh.2,113,327,761.00 na fedha za mfuko wa Jimbo ni Sh. 8,000,000.00.

Mh.Rc.Makalla alisema ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru "Vijana ni Nguvu Kazi ya Taifa washirikishwe na kuwezeshwa ",alisema Mkoa wa Mbeya Unathamini nguvu Kazi kubwa inayotolewa na Vijana katika Mkoa na Taifa ambayo kama itatumika vizuri itaweza kuongeza pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.


Hivyo ili kuwezesha nguvu Kazi hii kutumika ipasavyo serikali ya Mkoa imeweka mikakati ifuatayo, Kwanza Mkoa unashirikiana na Halmashauri zote kuwawezesha Vijana kuwa na maeneo ya kutendea Kazi ambapo jumla ya ekari 108 na maeneo 14 yametengwa.

Pili Kuzihamasisha Halmashauri kutenga asilimia 5 ya mapato ya ndani ambapo katika Mkoa mpaka sasa Jumla Sh. 887,928,422.00 zimetengwa kwa lengo la kuwawezesha Vijana,Tatu Kuunda Vikundi vya ujasiriamali vya Vijana ambapo jumla ya Vikundi 603 vimeundwa,Nne Kuviwezesha Vikundi vya Vijana ambapo jumla ya Shilingi 419,841,000.00 zimetolewa kuwezesha Vijana kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment