BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDOA NYINGI ZAVUNJIKA, SABABU ZAANIKWA.

 
Dar es Salaam.Takwimu za kuvunjika kwa ndoa zinaongezeka kwa kasi na sasa siyo kifo kinachowatenganisha wapendanao, bali sheria hulazimika kuchukua mkondo wake.

Idadi ya talaka zilizosajiliwa na Wakala wa Usajili wa Vizazi, Vifo, Talaka na Ndoa (Rita) kwa mwaka 2013/14 ni 99; mwaka 2014/15 zilikuwa talaka 150.

Kwa mujibu wa Rita licha ya kuwa ndoa nyingi zinavunjika, lakini hazivunjwi kisheria na talaka zinazotolewa ni batili kwa sababu hazitambuliwi na wakala huyo. 


Meneja wa Mawasiliano, Taarifa na Elimu kwa Umma wa Rita, Josephat Kimaro amesema kuachana kienyeji au kupeana talaka zisizotambuliwa na Rita kuna madhara lukuki, ikiwamo kukosa mirathi, kushindwa kuoa au kuolewa na kusababisha migogoro kwenye familia.MWANANCHI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment