BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TABIA ZA MNYAMA KIBOKO NA MAISHA YAKE

Kiboko (Hippopotamus amphibius) ni mamalia mkubwa wa familia ya Hippopotamidae. Nyumbani kwake ni bara la Afrika.

Huishi kwenye maji ya mito na maziwa lakini ana uwezo wa kutembea kwenye nchi kavu mbali na maji. Chakula chake ni majani.

Kimo cha mbegani kinafikia mita 1.5 na urefu wake hadi mita 4.5. Uzito wake ni kati ya kilogramu 2700 na 4500 kg. Hivyo kiboko inashindana na kifaru juu ya cheo cha kuwa mnyama mzito wa pili kwenye nchi kavu baada ya tembo. 


Akikimbia hufikia mwendo wa kilomita 48 kwa saa ingawa kwa muda mdogo tu. 

Viboko huishi majini na nchi kavu, hasa kwenye maziwa na mito ambako viboko dume huishi kwenye sehemu kubwa ya mto na jike na watoto 5 mpaka 30. Wakati wa mchana hubaki wametulia kwa kukaa ndani ya maji au matope; kuzaliana na kuzaa watoto vyote hutokea ndani ya maji. 

Hujitokeza nyakati za giza kula nyasi. Wakati viboko hupumzika pamoja ndani ya maji, wakati wa kula nyasi hutawanyika na hakuna mipaka.

Licha ya kufanana kimaumbile na nguruwe na wanyama wengine wenye kwato nne, wanyama ambao wanachimbuko moja la karibu la uhai ni "sesataseani", (nyangumi, porpoises nk.) ambako walitoka zaidi ya miaka milioni 55 iliyopita. 


Mnyama wa kale asili ya nyangumi na kiboko aligawanyika kutoka jamii nyingine za wanyama wenye kwato nne mnamo miaka milioni 60 iliyopita. Mabaki ya kale zaidi ya kiboko ni ya jenasi Kenyapotamus katika Afrika, wa tangu miaka milioni 16 iliyopita.

Kiboko anatambulika kwa kinywa na meno yake makubwa, mwili usio na nywele, miguu mifupi na umbo kubwa. Ni mnyama wa ardhi wa tatu kwa ukubwa akiwa na uzito (kati ya tani 1.5 na 3.5), nyuma ya faru mweupe (tani 1.5 mpaka 4 ) na tembo (tani 3 mpaka 7 ).


Licha ya umbo lake la kujaa na miguu mifupi, kiboko huweza kumshinda mbio binadamu kwa urahisi. 

Kiboko pia katika mbio fupi wanafikia mpaka kasi ya km 29/saa. Kiboko ni miongoni mwa viumbe ambao ni wakorofi kuliko wote an husemekana kama ni mnyama kali kuliko wote Afrika. 

Kuna kadiri ya viboko 125,000 mpaka 150,000 katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara; Zambia 40,000 na Tanzania 20,000 mpaka 30,000.

Viboko bado wapo kwenye tishio la kutoweka kutokana na kutoweka kwa uoto na ujangili kuwinda nyama yao na meno yao chonge ya vipusa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: