Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa onyo hilo bungeni jana wakati akijibu mwongozo uliokuwa umeombwa na Mlinga siku tatu zilizopita kuwa baada ya kupitia video za tukio hilo amejiridhisha kufanywa kwa kitendo hicho.
Jumatano hii, Mlinga aliomba mwongozo wa Naibu Spika akilalamikia kuwa Theonest alimvua barakhashia yake na kutoka nayo nje na kumsababishia mtikisiko wa kiakili na kumnyima sifa ya kuendelea kukaa bungeni.
“Nimepitia picha za video za matukio ya siku hiyo nimejiridhia ni kweli baada ya kusoma dua, waheshimiwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni walianza kutoka ndani ya Bunge.
“Wakati wakitoka mheshimiwa Theonest alipita karibu na sehemu aliyokaa mheshimiwa Mlinga Akamvua baraghashia na kisha akatoka nayo nje ya ukumbi,” alisema Dk Ackson.MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment