BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

10 WAJITOKEZA KUGOMBEA UONGOZO CHAMA CHA SOKA MANISPAA YA MORO

 
Juma Mtanda, Morogoro.
Chama cha mpira wa miguu wilaya ya Morogoro (MMFA) kinatarajia kupata viongozi wapya baada ya wagombea 10 kuchukua na kurudisha fomu katika nafasi mbalimbali za kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu utaofanyika Julay 10 mwaka huu mjini hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Katibu wa kamati ya uchaguzi huo, Rafu Lumbe alisema kuwa ni wagombea 10 ndio waliochukua fumo na kurejesha kwa lengo la kugombea nafasi mbalimbali za chama cha soka wilaya baada ya viongozi wa zamani kumaliza muda wao wa kukiongoza chama hicho.

Lumbe alitaja majina ya wagombea hao kuwa ni Emmanuel Kimbawa na Shomari Kunguge wanaogombea nafasi ya mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti likijitokeza jina moja pekee la, Hashi Saleh katika nafasi hiyo.

Alitaja nafasi nyingine kuwa ni Katibu kuu Mtendaji kukiwa na wagombea wawili, Geofrey Mwatesa na Kafale Maharagande anayetea kiti hicho wakati Mwakilishi wa mkoa ikigombewa mgombea mmoja pekee na Salum Mkolwe.

Nafasi nyingine ni Mwakilishi wa Vilabu ikijiteza majina mawili ya Seleman Mansoor na Ramadhan Wagala huku Kamati Tendaji kukiwa na mgombea mmoja Alex Bulengwa na nafasi ya Mwakilishi Wanawake ni, Jacqueline Jones.

“Uchaguzi umepangwa kufanyika Julay 9 mwaka huu na mpaka zoezi la uchukuaji fomu na kurudi ni wagombea 10 tu ndio waliojitokeza lakini katika nafasi ya Mweka Hazina na Msaidizi wake wamekosekana wagombea wa kugombea nafasi hizo hivyo zitakuja kujazwa hapa baadaye.”alisema Lumbe.

Lumbe alisema kuwa ukiachilia nafasi ya Mweka Hazina na Msaidizi wake kukosa wagombe, kumejitokeza katika nafasi ya upungufu ya wagombea nafasi ya Kamati Tendaji ambapo mpaka sasa kumejitokeza mgombea mmoja.
 

Wagombea 10 wataoingia katika uchaguzi mkuu wa chama cha soka wilaya ya Morogoro Julay 9 katika uchaguzi huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: