BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO MOTO ULIVYOTEKETEZA KIWANDA CHA NGUO CHA 21st CENTURY TEXTILES LTD MOROGORO.

Kiwanda cha nguo cha 21st Century Textile Ltd kilichopo kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro kikiwaka moto baada ya moja ya mashine ya kusokota nyuzi kutoa cheche moto kisha kuteketeza sehemu kubwa ya kiwanda hicho ulionza majira ya saa 12 asubuhi ya jana ambapo moto huo ulidumu kwa zaidi ya saa 12.
 
Juma Mtanda,Morogoro. 

Kinda cha nguo cha 21st Century kilichopo kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro kimeteketea kwa moto na baadhi ya mitambo ya kusokota nyuzi na malighafi na kusababisha hasara  ambayo mpaka sasa bado haijafahamika.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Clement Munisi, alieleza kuwa moto huo ulizuka jana saa 12:00 asubuhi katikamoja ya mashine ya kutengenezea nguo.

Munisi alieleza kuwa moto ulianza kwa kutoa cheche na wafanyakazi walijaribu kuuzima kwa kutumia kifaa maalumu cha kuzima moto (Fire extinguisher ) pasipo mafanikio.

"Moto umeunguza baadhi ya mitambo na malighafi zilizokuwa katika chumba kimoja katika kiwanda hicho na kusababisha hasara kubwa".alisema Munisi.

Munisi alisema moto huo uliendelea kuenea katika vyumba vingine na kusababisha baadhi ya nguo zilizokuwa zikiendelea kutengenezwa katika mitambo kuungua na kusababisha hasara ambayo hadi hivi sasa thamani yake bado haijafahamika.

Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Ramadhani Pilipili, alisema licha ya kikosi hicho kuwahi kufika katika eneo la tukio, miundombinu ya kiwanda hicho ni kikwazo katika kuukabili.

"Miundombinu ya kiwanda ni tatizo kutokana na kukosekana na eneo sahihi la kupitishi mipira ya maji na hivyo kulazimika kutumia muda mwingi kuvunja ukuta ili kufanikisha uzimaji,” alisema.

Alisema changamoto hiyo imepelekea uzimaji kuwa gumu, kwani eneo la moto ulikoanzia kuwaka halijafikiwa isipokuwa eneo la pembezoni.

Alitoa wito kwa uongozi wa kiwanda kuweka miundombinu ya mabomba juu ya paa ili ikitokea tena tatizo kama hilo iwe rahisi kutatua.

Naye mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini, alisema huu ni mwezi wa tatu tangu mojawapo ya mashine inayotumika kuzalishia nguo kuwa na tatizo la kutoa cheche na hivyo wafanyakazi kulazimika kuzima mara kwa mara inapoonekana inatoa cheche za moto kutaka kuleta madhara. 


Ofisa Mazingira wa kiwanda hicho, Anna Gervas, alisema wafanyakazi wa kiwanda hicho wako hatarini kukosa ajira kutokana na uharibifu uliosababishwa na moto huo jambo linaloweza kupelekea kiwanda hicho kufungwa kwa muda.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: