BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MARUFUKU HII INAWAATHIRI SANA MASHOGA WA TANZANIA.


Ndoa za jinsia moja ikifungwa, Picha ya maktaba
SERIKALI imepiga marufuku matumizi na usambazaji wa vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema hatua hiyo ni kwa ajili ya udhibiti wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema Serikali imezuia matumizi ya vilainishi hivyo kwa sababu vinachochea kuongezeka vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria za nchi.

“Ni kweli Serikali imezuia vilainishi hivyo kwa sababu ya kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

“Katika wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 wana maambukizi ya VVU.

“Katika nchi yetu hakuna sheria inayoruhusu uhusiano wa jinsia moja na kuendelea kusambaza vilainishi hivyo ni kama kuhalalisha vitendo hivyo… mila na desturi zetu haziruhusu uhusiano huo,” alisema.

Alisema pamoja na nia njema na jitihada baina ya wizara na wadau katika mapambano dhidi ya Ukimwi, imebainika baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za utendaji na kusambaza vilaninshi hivyo.
Waziri alisema kitu hicho ni kinyume na makubaliano waliyoyaingia na Wizara ya Afya.

Alisema wizara baada ya kubaini wadau ambao wamekuwa wakisambaza vilainishi hivyo, wadau hao wameahidi kukusanya vilainishi hivyo na kuviteketeza.

Wizara pia imekubali kushirikiana na wadau hao ili kuangalia kama kuna fedha ambazo zingetumika kununua vilainishi hivyo ziweze kupangiwa matumizi stahiki kulingana na vipaumbele vya wizara, alisema.

“Nahitaji hizo fedha zinazotumika kununulia vilainishi wanipe niweze kujengea wodi za kina mama na kununulia pamba na glovu kwa ajili ya kina mama wanaotaka kuifungua kuliko kuzipeleka huko,”alisema.

Alisema utafiti mbalimbali nchini umethibitisha kuwapo kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU na ni miongoni mwa makundi maalum yaliyo katika hatari zaidi ya maambukizi kuliko kiwango kilichopo ambacho kwa sasa ni asilimia 5.1.

Aliyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na wanawake wanaofanya biashara za ngono, asilimia 26.

Wengine ni watu wanaojidunga sindano za dawa za kulevya ambao ni asilimia 36 na wanaume wanaojihusisha na jinsia moja asilimia 23.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: