BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KITWANGA AJEREA KATIKA JIMBO LA MISUNGWI.

Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga akizungumza nyumbani kwake wilayani Misungwi mkoani Mwanza leo. Picha na Michael Jamson 

Mwanza. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amekutana na waandishi wa habari nyumbani kwake Misungwi leo akisema amerejea jimboni kufanya kazi ya kutumikia wapiga kura.

Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais John Magufuli kutokana na kuingia bungeni na kujibu swali akiwa amelewa, amesema sasa atakaa jimboni muda mrefu kuliko awali alipobanwa na shughuli nyingine ya uwaziri.

Tangu afukuzwe kazi, Kitwanga ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mwigulu Nchemba, hajaonekana hadharani wala kukutana na vyombo vya habari hadi hivi karibuni picha zake ziliposambazwa akikabidhi ofisi kwa Nchemba.

Kitwanga ni mbunge wa jimbo la Misungwi kupitia CCM.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: