BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MHARIRI MTENDAJI NA MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI WAITWA NA JESHI LA POLISI.


Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga (kushoto) na mwandishi wake, Elias Msuya

Dar es Salaam.
Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga na mwandishi wake, Elias Msuya wameitwa na polisi kuhojiwa kuhusu makala iliyochapishwa na gazeti hilo kuhusu utendaji wa jeshi hilo.

Wakati Msuya alipigiwa simu jana na kuhojiwa leo asubuhi kuhusu makala aliyoandika, Sanga ameitwa leo na tayari ameondoka ofisini kwake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito huo. 


Makala hiyo ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Polisi na Hofu ya Watawala Kuondoka Madarakani”, ilichapishwa na gazeti hilo jana.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: