BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATOTO WANAONYONYA VIDELE HUPATA FAIDA YA KUIMARISHA KINGA YA MWILI.

 
Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pediatrics, huo ni usafi dhanio,kwani yatokanayo na baadhi ya wadudu huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana kuzuia baadhi ya alergy.

Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi thelathini na mbili,walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand.

Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.

Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano na kumi na moja na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye umri kati ya miaka kumi na tatu na thelathini na miwili.

Huku thuluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Watoto wanaoweza kupata matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani (alergy) kutokana na vitu kama vumbi kutoka majumbani,manyoya ya paka au mbwa, lakini watoto wenye kunyonya vidole gumba na kung’ata kucha walikuwa ni chini ya theluthi moja kuliko watoto wenye tabia hii ya unyonywaji vidole.

Na tabia hii ya unyonyaji vidole au ung’ataji kucha inaonekana kuwa kinga mpaka wanapofikia umri wa utu uzima.

" kuwa na paka au mbwa majumbani,ndugu au jamaa wanaofanya kazi mashambani pia imeonekana kuwa ni sababu kubwa inayosababisha mazingira ya ukuaji wa magonjwa yanayosababishwa na

kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: