BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WAMGUNDUA MTU ALIYEBAKA NA KUMUUA MSICHANA (17) BAADA YA MIAKA 34 KUPITA LAKINI HII NDIO HUKUMU KWA MBAKAJI.


Mwanaume aliyebaka na kuua msichana mmoja mwaka wa 1982 amehukumiwa kifungo cha maisha jela .

Alipataikana vipi miaka 34 baadaye ?
James Warnock, 56, alimbaka na kumnyonga binti huyo mwenye umri wa miaka 17 wakati huo Yiannoulla Yianni.

Mauji hayo yaliitamausha mji wa Hampstead.

Mweka rekodi za umma za chemechembe za DNA katika mji wa London Uingereza, Nicholas Hilliard QC aliieleza jopo la majaji wa Old Bailey kuwa bi Yianni alipitia mateso ya kutisha alipokuwa mikononi mwa mshukiwa.
James akijitetea kwa kuiambia mahakama kuwa alikuwa na uhusiano wa kisiri na binti huyo Yiannoulla Yianni.

Yamkini Warnock alitishia kumuua binti huyo kabla ya kumbaka.

Lakini hata baada ya kukamilisha haja na tamaa yake ya mwili alimuua binti huyo aliyekuwa anaishi katika mtaa mmoja naye takriban mita mia tano kutoka makao yake.

Warnock aliendelea kuishi katika mtaa huohuo kwa sababu hakuna aliyemuona akitekeleza unyama huo, na polisi hawakuwa na sababu ya kumshuku.
James na Yianni walikuwa wanaishi katika mtaa mmoja.

Kwa miaka 34 hakuna aliyejua aliyetekeleza mauaji hayo alikuwa mmoja wao hadi majuzi tu, polisi walipomkamata akisambaza picha za utupu za watoto.

Kama ilivyoada alilazimika kutoa manii yake na mate kwa chembechembe za DNA.

Na walipofanya vipimo na kutafuta miongoni mwa kesi ambazo hazijatatuliwa, walipigwa na butwaa kupata kuwa alikuwa na chembechembe za manii sawa na ile iliyopatikana karibu na ulikopatikana mwili wa binti huyo Yiannoulla Yianni mwaka wa 1982.

Papo hapo polisi walijua kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo.

Jaji Hilliard alimhukumu akihoji kwanini binadamu ni wanyama kiasi hicho?

Kosa hilo lilipotendeka matumizi ya teknolojia ya DNA katika kuvumbua kesi mbalimbali haikuwepo na hivyo kutattua moja ya kesi za mauaji iliyobakia bila majibu kwa familia ya muathiriwa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: