BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI APOKEA KWA MSTUKO TAARIFA ZA AJALI YA MAGARI NJIAPANDA YA DUMILA NA VETA ILIYOUA WATU 12 MORO

Lori lilikuwa limebeba mpunga likizimwa moto na askari wa kikosi cha Zimamoto baada ya kutokea ajali ya magari matatu kugongana kwa nyakati tofauti katika eneo la njiapanda ya Dakawa - Veta, Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro katika Barabara Kuu ya Morogoro- Dodoma na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine kujeruhiwa.PICHA/MTANDA BLOG
 
RAIS John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu 12 waliopoteza maisha katika ajali mbili zilizotokea katika eneo moja la Veta Dakawa tarafa ya Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa 11:30 jioni ya Juni 30 mwaka huu, ambapo watu watano walikufa papo hapo, baada ya malori mawili, mojawapo likiwa na shehena ya mafuta, kugongana na kuwaka moto na
lingine lililokuwa limebeba mpunga.

Ajali ya pili ilitokea hapohapo majira ya saa 10:00 alfajiri ya Julai mosi mwaka huu, baada ya basi la kampuni ya Otta High Class, kupamia lori la mafuta lililokuwa likiungua moto na kusababisha vifo vya watu saba mpaka jana.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza jana kuwa katika salamu hizo kwa wananchi waliofikwa na msiba huo, kupitia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe, Rais Magufuli alisema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa hizo. Alisema Taifa limepoteza nguvu kazi muhimu, na ndugu, jamaa na marafiki wamepoteza watu waliwaotegemea.

“Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Steven Kebwe, naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wote waliopatwa na msiba na uwaambie naunga nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. “Pia nawaombea wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu na Mwenyezi awapumzishe marehemu wote mahali pema peponi, amina,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia aliwaombea majeruhi wote waliolazwa hospitalini na wale wanaoendelea kupata matibabu wakiwa nyumbani, kupona haraka ili waendelee na kazi zao za kila siku.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: