Askari
kata ya Uwanja wa taifa Manispaa ya Morogoro, Mbaraka Mahanyu kulia na
afisa ustawi wa jamii wa kata hiyo kushoto wakimpeleka mkazi wa mtaa wa
Kiswanya B, Farida Ghumpi (34) kituo cha polisi baada ya kudaiwa
kumtumikisha mwanafunzi wa shule ya msingi Mwau kijiji cha Ikungi
Singida anayedaiwa kusoma darasa la tano, Shaminu Iddi (12) kazi za
ndani, kabla ya kitengo cha dawati la jinsia cha jeshi polisi kumwamuru
kumlipa mtoto huyo stahiki zake ikiwemo kiasi cha Sh75,000 kisha
kumrudisha kijijini kwao.
Mafundi
selemala katika kalakana iliyopo eneo la Fire kata ya Sabasaba Manispaa
ya Morogoro wakiendelea na kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa
kutumiwa na wanafunzi, mkoa wa Morogoro una upungufu wa madawati 73,972
kwa shule za sekondari na msingi.PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akizungumza jambo na watumishi mbalimbali wa idara za serikali katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro, kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Dk Steven Kebwe na kulia ni mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina ChonjoMmoja wa watumishi akitoa kero kwa waziri
Baadhi ya wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Morogoro kutoka kushoto, Siriel Mchemba (Gairo), Regina Chonjo (Morogoro), Mohamedi Utaly (Mvomero) na Jacob Kassema (Ulanga) wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa juu ya kuwepo kwa watumishi hewa 315 huku wilaya ya Kilosa ikiongoza kwa kuwa na watumishi hewa 98 na zoezi la utengenezaji wa madawati ulioagizwa na rais John Magufuli.
0 comments:
Post a Comment