Utawala nchini Uturuki umevamia kambi za kijeshi kote nchini kuwatafuta wanajeshi wanaoshukiwa kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyozimwa siku ya Ijumaa.Katika oparesheni kwenye mji ulio magharibi wa Denizli saa chacha zilizopita kamanda mmoja wa kikosi cha jeshi na zaidi ya wanajeshi 50 walikamatwa.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini amesema kuwa jeshi limerejesha udhibiti katika asilimia kubwa ya kambi za kijeshi japo kuna baadhi ambazo zipochini ya usimamizi ya wale waliunga mkono mapinduzi.
Majaji takriban 3000 ambao wanatuhumiwa kupinga serikali ya rais Reccep Teyyip Erdogan wamesimamishwa kazi.Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema kuwa bunge litaamua ikiwa litabuni sheria ya hukumu ya kifo.
Wale waliokamatwa wanatajwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini raia wa Uturuki anayeishi nchini Marekani Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kwa kupamnga mapinduzi hayo.BBCWanajeshi waasi 104 wauawa Uturuki
Julai 16/2016.Naibu mkuu wa jeshi la Uturuki ametangaza kwa njia ya runinga kuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi limeshindwa.
Jenerali Umit Dundar alisema kuwa wapanga mapinduzi 104 wameuauwa. Pia amesema kuwa watu wengine 90 wakiwemo polisi na raia wameuawa.
Usiku kucha miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.
Maafisa wanasema kuwa zaidi ya wanajeshi 1500 wamekamatwa huku wale wa vyeo vya juu wakiwemo majerali wakipokonywa nyadhifa zao.

0 comments:
Post a Comment