BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA MANISPAA YA MORO WAOTA MBAWA KISA KUENGULIWA MGOMBEA.

 
Juma Mtanda,Morogoro
Chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA) kimepitisha majina ya wagombea nane baada ya baraza la mitihani la taifa (Necta) kumaliza kazi ya kuhakiki vyeti tisa vya elimu ya wagombea huku jina la mgombea mmoja likienguliwa kutokana na kukosa sifa za kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ambao ulipangwa kufanyika leo Julay 17 umesongezwa mbele baada ya wajumbe wa mkutano mkuu kuweka pingamizi zinazodaiwa kamati huru ya uchanguzi huo kukiuka taratibu ikiwemo kuenguliwa kwa jina la mmoja wa wagombea.


Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Katibu wa kamati huru ya uchaguzi huo, Rafu Lumbe alisema kuwa ni majina nane pekee ndio yaliyoruhusiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea uongozi MMFA huku mmoja wa mgombea katika nafasi ya mwenyekiti akiondolewa kwa kukosa sifa.

Lumbe alisema kuwa mgombea huyo ameenguliwa kutokana na cheti chake kuwa na kasoro yaliyojitokeza katika uhakiki ambapo vilipelekwa katika baraza la mitihani la taifa hivyo kutokana na kasoro hizo, majina yaliyoruhusiwa kuendelea na mchakato wa kugombea uongozi kwa nafasi walizoomba mpaka sasa ni nane pekee.

Uchaguzi huo umepangwa kuafanyika Julai 17 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuanzia majira ya saa 3:30 asubuhi sasa umeota mbawa kutokana na pingamizi hilo hadi hapo watakapopanga siku ya uchaguzi.

Kauri hiyo ilitolewa na Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Astaria Mwang'ombe kufuatia kikao cha pamoja cha kamati huru ya uchaguzi na wagombea kilichofanyika jana.


Lumbe alitaja majina ya wagombea hao wanaendelea na mchakato kuwa ni, Emmanuel Kimbawa anayegombea nafasi ya mwenyekiti wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Hashi Saleh huku nafasi ya Katibu kuu Mtendaji ni, Geofrey Mwatesa na Kafale Maharagande ambaye anatetea kiti hicho na Salum Mkolwe akigombea nafasi ya Mwakilishi wa mkoa.

Kwa upande wa nafasi ya Mwakilishi wa Vilabu ni, Seleman Mansoor na Ramadhan Wagala wakati katika nafasi ya Kamati Tendaji, Alex Bulengwa na nafasi ya Mwakilishi Wanawake ni, Jacqueline Jones.

“Uchaguzi umepangwa kufanyika Julay 17 mwaka huu ukumbi wa Manispaa na sasa wagombea nane ndio wameruhusiwa kuanza kampeni baada ya vyeti vya elimu zao kuhakikiwa na Necta, isipokuwa mgombea mmoja nafasi ya mwenyekiti jina lake limeenguliwa kwa kukosa sifa.”alisema Lumbe.

Lumbe alisema kuwa mpaka sasa kuna nafasi zipo wazi kutokana na kukosa wagombea ikiwemo ya Mweka Hazina na Msaidizi wake na nafasi ya Kamati Tendaji ambayo mpaka sasa kumejitokeza mgombea mmoja na kuwa nafasi hizo zitajazwa hapa baadaye.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: