BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO WA KIKE WA MIAKA SITA AWEKEWA BETRI KATIKA MOYO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI TANZANIA


TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imefanya upasuaji mwingine kwa mafanikio kwa kuweka betri katika moyo wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita.

Operesheni hiyo imefanywa kwa kushirikiana na Chuo cha Madaktari Bingwa wa Moyo cha Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, daktari bingwa wa moyo kutoka katika taasisi hiyo, Dk Michael Valentine, alisema upasuaji huo wa aina yake, umefanywa na jopo la madaktari bingwa wa moyo.

“Napongeza madaktari wa moyo wa JKIC waliofanikisha upasuaji huo,” alisema na kuongeza kuwa chombo hicho kilichowekwa katika moyo, kitasaidia moyo wa mgonjwa huyo kufanya kazi vyema na yeye kuishi maisha ya kawaida.

“Ni matumaini yetu, mtoto huyo wa kike ataishi umri mrefu,” alisema Dk Valentine na kuongeza kuwa wagonjwa wawili waliokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, wamekabidhiwa kwa madaktari hao.

Kifaa hicho kidogo huwekwa katika kifua cha mgonjwa ili kusaidia mapigo ya moyo ya mgonjwa kuwa ya kawaida ambapo Dk Valentine alisema kinapaswa kubadilishwa baada ya miaka kumi.

“Mgonjwa anahitaji kifaa hiki kama moyo wake unasukuma damu kwa kasi au polepole. Katika hali hiyo, mwili hukosa damu ya kutosha na kusababisha mgonjwa kuchoka, kupoteza fahamu, kupata uoni hafifu na kushindwa kupumua,” alisema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: