BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYAKAZI WAPEWA LIKIZO ILI WAKATAZAME FILAMU KATIKA KUMBI

Wafanyakazi wengi kusini mwa India wamepewa likizo kwa sababu ya filamu ya mwigizaji filamu inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema jana na filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth.

Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile kwamba wanaugua ili wasifike kazini.

Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu.

Filamu hiyo kwa jina Kabali ilionyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema hiyo jana.

Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.

Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki zake.

Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.

Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya kampuni zilitangaza siku ya jana Ijumaa kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.

Kampuni moja inasema imechukua hatua hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya jana.
 

Rajinikanth mwenye umri wa miaka 65, ameigiza katika filamu zaidi ya 170, nyingi katika lugha ya Kitamil.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: