Dar es Salaam. Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku wa jana kwa kupigwa risasi wakati akiwa eneo la kazi la Sayansi Kijitonyama katika mkoa wa Dar es Salaam.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime alieleza kuwa askari huyo alipigwa risasi majira ya saa 2 usiku na chanzo cha mauaji hayo bado hayajafahamika.
“Tumempoteza askari wetu lakini mpaka sasa bado hatujapata chanzo na tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo.” alisema Kamanda Fuime.
0 comments:
Post a Comment