BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA AGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA BAADA YA KUIHAMA CCM

 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye mwaka jana alijiunga na upinzani, amesema nafasi ya uenyekiti wa Kanda ya Pwani anayogombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inampandisha hadhi kwa sababu anakiimarisha chama hicho tofauti na wengi wanavyodhani kuwa itashusha hadhi yake.

Sumaye alizungumza jana baada ya kurudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Ofisi za Kanda iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alisema chama hicho kwa hivi sasa kinatakiwa kuimarishwa kuanzia chini ili kukidhibiti chama tawala, CCM, ndio maana ameamua kugombea nafasi hiyo.

“Nafasi ninayogombea ya uenyekiti wa kanda inanipandisha hadhi kwa sababu nafasi hii ni muhimu kwenye kanda. Hiki chama chetu kinatakiwa kuimarishwa huku chini,” alisema Sumaye aliyepokea fomu hiyo juzi kutoka kwa wanachama wa Chadema baada ya kumshawishi.

Sumaye aliyerudisha fomu hizo jana katika ofisi hizo za kanda huku akisindikizwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanachama hao walimpima na kumwona anatosha katika nafasi hiyo ndio maana alikubali, hivyo alisisitiza msimamo wake wa kuondoka CCM kuwa ni kutafuta demokrasia ya kweli kutoka upande mwingine.

"Ili kuwe na demokrasia ya kweli lazima kuwe na vyama vikubwa viwili vya siasa vinavyoshindana. Hapo wananchi watafurahi. Nataka tufike mahali watanzania wachague viongozi wanaowataka," alisema Sumaye na kuongeza kuwa habari ya kung'ang'ania chama kimoja haileti maendeleo ya kweli wala demokrasia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jimbo la Ilala, Allen Mazoko alisema kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Jimbo la Ukonga, Swaya Rajab na Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani, Baraka Mwago walimshawishi Sumaye kugombea nafasi hiyo, sababu yao ya msingi ilikuwa ni hali ya kisiasa iliyopo Mkoa wa Pwani.

Katibu wa Kanda ya Pwani, Casimir Mabina alisema chama hicho kina kanda nane, hivyo uongozi wa taifa hivi sasa upo katika hatua za kuimarisha kwa kufanya chaguzi.

Alisema kwa upande wa kanda hiyo jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo ambapo mpaka saa saba mchana nafasi ya uenyekiti ilikuwa inawaniwa na watu watatu.

Mbali na Sumaye wengine ni Gango Kidela (Mwenyekiti Segerea) na John Guninita. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa na watu watatu; Thomas Nyahende, Adolf Mkono na Said Kubenea (Mbunge wa Ubungo).

Nafasi ya Mweka Hazina inagombewa na Makongoro Mahanga, Florence Kasilima na Lucy Mageleli. Alisema siku ya uchaguzi itapangwa na Kamati Kuu ya chama hicho.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: