JESHI LA POLISI LINAWEZA KUKUSANYA SH2.7BIL KWA MWEZI KUPITIA KWA BODABODA PEKEE.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani Manispaa ya Morogoro akiwa amemkamata mwendesha pikipiki baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani wakati wa operesheni ya kuwakamata madereva wa pikipiki wasiozingatia sheria za usalama barabarani.Picha/MTANDA BLOG
Juma Mtanda, Morogoro-jphtjuma@gmail.comz
Jeshi la Polisi linaweza kuliingizia taifa kipato kisichopungua Sh2.7 bilioni kwa mwezi kutokana na tozo za faini zinazotokana na makosa ya Usalama barabarani kwa upande wa Tanzania Bara pekee.
Kwa mfano kwa wastani wa makosa 100 yanayofanyika kwa mwezi mmoja yanaweza kukusanya faini ya zaidi ya Sh Milioni 900 kwa kiwango cha chini cha faini ya Sh 30,000 kwa kosa moja la usalama barabarani.
Kutokana na tozo za faini hizo kwa mikoa mikoa 30 yenye wilaya 139 serikali itakuwa imepata kiasi hicho cha fedha au zaidi na pesa hizo kupelekwa katika matumizi mengine ya huduma za jamii ikiwa ni pamoja na maboresho ya jeshi hilo.
Zaidi ya serikali kupata kiasi hicho cha fedha lakini pia jeshi la Polisi linaweza kutumia njia hiyo kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva mambumbu wasiozitambua sheria za usalama barabarabani ambao kila kukicha wamekuwa wakipata ajali zinazoweza kuepukika.Mwendesha pikipiki akiwa amepakia abiria watatu kinyume na sheria za usalama barabarani.
Adhabu hizi pia zinatoa fundisho kwa madereva wasiotii sheria za usalama barabarani na hivyo kutumika kama njia ya kuwanyoosha madereva wakorofi.
Moja ya eneo korofi ambalo kwa sasa linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani ni pamoja na zile zinazochangiwa na Pikipiki au Bodaboda adhabu na Elimu ya Usalama barabarani vikienda kwa pamoja utasaidia kuwarejesha madereva hawa kwenye mstari na pia kupunguza ajali za mara kwa mara
Sheria kali inabidi zichukuliwe kwa madereva wote wa magari na bodaboda ambao wamekua wakifanya makosa ya makusudi kama vile kupakia upakiaji wa abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki maarufu kama mishkaki.
Kupakiza watoto wadogo wenye chini ya umri ya miaka (9), kubeba mizigo kupita kiasi inayosababisha dereva kushindwa kuona nyuma kwa kutumia vioo vya pembeni (side mirror).
Dereva kuendesha pikipiki pasipokuwa na mafunzo na chombo hicho lakini jambo lingine baadhi ya madereva wa pikipiki wamekuwa na tabia ya kuharibu mfumo wa bomba la kutolea moshi Eksozi na kutoa muungurumu kama pikipiki za mashindano na kusababisha kero kila inapopita.
Makosa yanayofanywa na waendesha bodaboda ambao wengi wao wamejikita katika biashara wamekuwa wakikumbwa na mikasa mbalimbali ambayo serikali inapaswa sasa kuingilia kati ili kunusuru kundi hilo ambalo limekuwa tegemeo kwa taifa na kuendesha familia kwani wanapopata matatizo kundi hilo familia zimekuwa zikiyumba kiuchumi na mahitaji muhimu.
Kwa takwimu za mkoa wa Dar es Salaam pekee zinaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2011 hadi Juni 2015, watu 514 walifariki dunia na wengine 10,079 wajeruhiwa kutokana na pikipiki 10,351 kupata ajali za chombo hicho.
Kwa mwaka 2014, ndiyo mwaka ambao ulikuwa mbaya zaidi kwa waendesha bodaboda baada ya kutokea kwa vifo vya watu 160 huku 1,768 wakijeruhiwa kutokana na ajali 2,082 za pikipiki ambapo hapo tunaweza kuona namna taifa inavyopoteza nguvu kazi na familia ujumla.
Hali hiyo inatokana na ukosefu wa madereva kutopata mafunzo stahili hasa katika chuo vya Veta ambavyo itakuwa rahisi kupata mafunzo na gharama nafuu.
Ukiachilia mbali madereva wa pikipiki kukumbwa na vifo, vilema vya kudumu kutokana na kupata ajali, madereva hao wanaweza kupatwa na ugonjwa wa homa ya mapafu, kwa mapafu kujaa maji kutokana na dereva wa pikipiki kuendesha kwa muda mrefu bila kuvaa koti la kujinga na upepo mkali (Jacketi).
Ugonjwa mwingine wanaoweza kumpata dereva ni kifua kikuu (TB) unaotokana na dereva kukusanya virus vingi vilivyopo hewani kwa njia ya mdomo na pua ambapo kinga yake ni kuvaa kofia ngumu (Elment) na kuvuta moshi wa magari.
Lakini kupakiaji abiria zaidi ya mmoja (Mishikaki) dereva pia yupo katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kupungukiwa na nguvu za kiume kwani humlazimu dereva kukaa eneo la tanki la mafuta pia kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa viungio vya uti wa mgongo.
Kwa takwimu za kitaifa ndani ya kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2010 hadi Desemba 2014 watu 3,825 walifariki dunia kwa ajali za pikipiki nchini na watu 21,236 walijeruhiwa kuanzi Januari hadi Juni kwa mwaka 2015.
Kipindi cha Januari hadi Juni mwaka 2015 ajali za pikipiki pekee zilitokea 1,352 na kusababisha vifo vya watu 473 na kujeruhi 1,275.
Baadhi ya mikoa waendesha pikipiki za biashara wamekuwa wakitumika katika uhalifu yakiwemo matukio ya kupora simu kwa watu wanaotembea kwa miguu kando ya barabara nyakati za jioni ikiwemo mkoa wa Morogoro.
Jeshi la polisi linaweza kudhibiti matukio hayo kwa kuendesha zoezi maalumu la operesheni ya kukamata pikipiki zote na kuzikagua kwani watagundua mambo mengi.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment