BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA URAIS AMCHAGUA MKE WAKE KUWA MGOMBEA MWENZA


Rais wa Nicaragua Daniel Ortega amemtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwengine.

Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhfa maarufu wa msemaji wa serikali na anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe.

Amekuwa akionekana katika runinga ya Nicaragua kila siku

Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao cha kibinafsi.

Rais Ortega akiwa hazungumzi sana katika vyombo vya habari ,mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga akijadili sera na kujikuza .

Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo anajua kuongea Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi.

Pia anasifa za kuvaa mavazi yenye rangi nyingi na vito vya miaka ya sitini.

Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo wanamuona bi Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika taifa lake kutokana na hadhi yake katika uma.

Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri wakili wa chama chao cha Sandinista.bbc
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: