BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MUZIKI WA TAARABU WAPATA PIGO TANZANIA.


Msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Shakila Said wakati wa uhai wake.

Dar es Salaam. Msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Shakila Said amefariki dunia nyumbani kwake, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo cha msanii huyo nyota mwenye umri wa miaka 70 zilianza kusambaa mitandaoni usiku, na kuhamia katika vituo vya redio mbalimbali ambazo zilianza kucheza muziki wa mkongwe huyo ambaye wakati wa uhai wake alibahatika kuzaa watoto 15 na 12 wakiwa hai. 


Kwa mujibu wa taarifa za kifo cha mtunzi wa nyimbo na mwimbaji wa kundi la JKT Taarab, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ukisubiri taratibu za mazishi. 

Shakila alianza kujiingiza katika kazi ya muziki tangu mwaka 1961 akiwa na umri wa miaka 15.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: