BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NANI ANASEMA SABODO ANA FEDHA ZA KUISAIDIA SERIKALI YA JPM KUHAMIA DODOMA ?.



Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.

“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” alisema Sabodo na kuongeza: “Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. 


Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: