BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE KUBWA ZAIDI DUNIANI YENYE UWEZO WA KUJIGEUZA KUWA MELI KATIKA MAJI YAPAA ANGANI


Safari ya ndege ndefu zaidi dunian imeanza nchini Uingereza baada ya majaribio ya awali kufutwa dakika za mwisho.

Ndege hiyo inayojulikana kama Airlander 10, ambayo ni ndege na pia meli, ilitoka uwanja wa Carding
ton huko Bedfordshire.
Ndege hiyo ya gharama ya pauni milioni 25 ina urefu wa mita 93, ni refu kwa mita 15 zaidi ya ndege yoyote kubwa ya abiria.Ndege hiyo hairuhusiwi kuruka usiku inapofanyiwa majaribio.

Ndege hii iliundwa kwanza kwa serikali ya Marekani kama ndege ya kufanya ujasusi lakini mradi huo ukafutwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Kisha kampuni ya uingereza ya Hybrid Air Vehicles (HAV) ikazindua kampeni ya kufanikisha mradi huo.

Ndege hiyo ina uwezo wa kusalia angani kwa takriban siku tano.

Kampuni ya HAV inasema ndege hiyo itatumiwa kwa masuala kadhj yakiwemo ujasusi, mawasiliano, kusafirisha misaada na hata abiria.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: