BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 36 WANYONGWA

Makuruti waliouawa na wapiganaji wa Islamic State 2014
Iraq imewanyonga wapiganaji 36 wa kundi la Islamic State wanaohusishwa na mauaji ya makurutu 1,700 katika kambi moja iliokuwa ya Marekani mwaka 2014.

Mauaji hayo katika kambi ya Speicher karibu na Tikrit yalifanywa na wapiganaji kutoka Islamic State ilipochukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Iraq.

Hisia kali zilizotolewa kufuatia mauaji hayo ya raia wa Kishia zilichochea kubuniwa kwa kundi la wapiganaji wa Kishia katika vita dhidi ya Islamic State.

Wapiganaji wa Islamic State walitoa picha na video wakionyesha mauaji hayo ya 2014.

Makaburi ya halaiki yalifichuliwa mwaka mmoja baadaye.Makaburi hayo yaligunduliwa baada ya wanajeshi wa Iraq kulikomboa eneo hilo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: