BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PICHA YA MVULANA NCHINI SYRIA ILIYOSIKITISHA WENGI BAADA YA SHAMBULIO AKIWA AMEJAA DAMU NA VUMBI

Mvulana Omran mwenye umri wa miaka minne
Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la kubebea wagonjwa Syria, imeweka wazi tena madhila wanayopitia raia nchini Syria.

Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.

Picha hiyo ya Omran, 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana katika ufukwe wa Uturuki mwaka jana.

Omran alitolewa kwenye vifusi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la kutoka angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.

Jamii ya kimataifa imeguswa na wito wa kusitishwa kwa mapigano kutolewa.

Mshirika mkuu wa Rais Bashar al-Assad, Urusi, imesema iko tayari kusitisha vita katika mji huo wa kaskazini kwa saa 48 kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia.
Mwili wa Ayran Kurdi ukiondolewa kwenye ufukwe wa bahari Uturuki mwaka jana"Nimepiga picha nyingi za watoto waliouawa au kujeruhiwa wakati wa mashambulio yanayotekelezwa kila siku," mpiga picha hiyo Mahmoud Rslan aliambia AFP.

"Kawaida, huwa wamepoteza fahamu au wanalia. Lakini Omran alikuwa amekaa hapo, bila kutamka neno, akionekana kuduwaa, kana kwamba hakuwa anafahamu nini kilichokuwa kimetokea."

Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini Syria.

Zaidi ya watu 17,700 wanakadiriwa kufariki wakiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: