SAYANSI NDANI YA KITABU KITAKATIFU NA MIUJIZA YAKE
KUPULIZIWA ROHO "MTOTO" AKIWA NDANI YA TUMBO LA MAMA YAKE NA KUPITISHWA QADAR JUU YAKE.
Hatua ya tatu ya ukuaji wa mtoto ndani ya tumbo la mama yake"Mudhgha" humalizika pindi tu itimiapo wiki ya sita au siku 42 baada ya mimba kutunga, hapa hufanyika tukio kubwa na la kihistoria pasina mama wala kiumbe anaye kuwa ndani yake kujua.
Ni tukio la kupuliziwa roho ili kiumbe awe mwenye mwili na roho.
Kwa mujibu wa hadithi ya mtume Muhammad (s.a.w) iliyosimuliwa na Abdallah Ibn Mas'ud (RA)-mtume (s.a.w) anasema:-
``Kila mmoja wenu huumbika tumboni mwa mama yake siku arobaini na huwa Alaqah, kisha huwa Mudhgha na kisha Allah (swt) anamtuma malaika (juu ya mtoto aliye tumboni) na kumuamrisha kuandika juu lake mambo makuu manne:-
(01) Riziki yake (ya duniani)
(02) Umri wake (wa duniani)
(03) Ajari yake (ya duniani)
(04) (Na kama atakuwa) mwema au muovu (duniani) kisha hupuliziwa roho.
Na naapa kwa Mola "kwamba" mmoja wenu anaweza kufanya a'ammal za watu wa motoni hadi isibakie baina yake na moto ila shibri moja tu ya kusadifu yaliyo andikwa (na malaika) katika kitabu chake na akageuka kufanya a'ammal za watu wa peponi na kuingia peponi.
Mtu anaweza kufanya a'ammali za watu wa peponi hadi pasibakie baina yake na pepo ila shibri moja tu ya kusadifu yaliyo andikwa na (malaika) katika kitabu chake akafanya a'ammali za watu wa motoni na akaingia motoni (Imamu Muslimu).
Hivyo basi, kwa kupuliziwa roho siku ya arobaini na mbili huu ndio unakuwa mwisho wa hatua ya tatu ya ukuaji wa mtoto ndani ya tumbo la mama yake yaani (Mudhgha),baada ya hapo huungia hatua ya kutengenezwa mifupa (the bone formation) ambayo pia Qur-an imeitaja.
0 comments:
Post a Comment