Wafamasia wa Chuo Kikuu cha Muhimbili Dar es Salaam wameelezea na kuthibitisha kisayansi kuwa supu ya samaki aina ya pweza inaweza kuchochea hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume.
Kwa miaka mingi ilikuwa ikiaminika na watu wengi hasa wa ukanda wa pwani ya Tanzania na Afrika Mashariki kuwa supu hiyo inaongeza hamu ya kufanya mapenzi lakini kulikuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi wa kuunga mkono madai hayo
''Sio kitu cha imani tena, sasa hivi tuna ushahidi wa awali unaotupa mwanga wa matumaini kuthibitisaha matokeo hayo katika mwili wa binadamu kwa utafiti zaidi''
alisema Profesa Eliangiringa Kaale mkuu wa kitengo cha utafiti na ukuzaji wa maabara katika Chuo Kikuu cha Muhimbili shule ya Famasia ambaye pia alishiriki kusimamia utafiti huo.
Utafiti huo ulifanywa na wanafunzi na wasimamizi wa famasi kwa panya dume.
Hata hivyo Profesa Kaale alionya wanywaji wa supu ya pweza kuwa matokeo ya utafiti huo hayamaanishi kuwa tiba ya kuponyesha matatizo ya kushindwa kufanya ngono kwa wanaume imepatikana
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ SAMAKI AINA YA PWEZA ATHIBITISHWA KISAYANSI KUWA NI KICHOCHEO KWA WANAUME KUFANYA MAPENZI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment