BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKWELI KUHUSU SAMAKI AINA YA NGUVA JE NI KWELI SAMAKI MTU ?


 

Na Geofrey Chambua.Mnyama aina ya Nguva ambaye watu wamekuwa wakimwelezea kwa namna tofauti tofauti na endapo mazingira ya bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho kutoweka, mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu mnyama huyo si ya kweli.

1. Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe. Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake.

2. Nguva ni mnyama anayezaa na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine na wakati akinyonyesha husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

3. Mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto mmoja pekee hivyo nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho ima kuweka kwenye maeneo tengefu

4. Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000.

5. Alikuwa akionekana Dar es Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena kwani ni mnyama mwenye aibu sana na anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huhama na kwenda mbali zaidi kwenye utulivu

6. Kuna simulizi za ajabu ajabu kuhusu huyu samaki; kwa mfano wanasema kwamba mvuvi akimvua lazima kwanza afanye naye tendo la ndoa kama tambiko.(Baby Born With Mermaid Tail)
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: