BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VINYAGO VYA UTUPU VYA MGOMBEA URAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP VYAWAVUTIWA WATU.

Watu wakipiga selfie na vinyago vya Donald Trump New York 18 Agosti 2016Huu hapa ni mkusanyiko wa picha kutoka Marekani, ambapo vinyago vya utupu vya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump viliwavutia sana wapita njia.

Vinyago vya utupu vya Donald Trump viliwekwa maeneo mengi ya miji ya New York, Los Angeles, Seattle, San Francisco na Cleveland nchini Marekani mnamo Alhamisi na kuwavutia sana watu
Wafanyakazi wa New York City Parks wakikagua kinyago cha Trump eneo la Union SquareVinyago hivyo vinavyomuonesha Trump akiwa na sura ya ukali viliwekwa chini ya mradi wa INDECLINE, na viliundwa na msanii kutoka Cleveland.Watu wakitazama kinyago cha Trump mjini San Francisco"Ni kupitia vinyago hivi ambapo tunaonesha umma sura na sifa halisi ya mmoja wa wanasiasa wabaya na wanaochukiwa zaidi Marekani," INDECLINE walisema kupitia taarifa.Mwanamke akipiga busu kinyago cha Donald Trump mjini San FranciscoWapita njia wengi walivutiwa na kufurahishwa na vinyago hivyo, baadhi wakiamua hata kuvibusu.Wafanyakazi wa New York City Parks wakiondoa kinyago cha Donald TrumpLakini wafanyakazi wa bustani na maeneo ya umma New York waliondoa vinyago hivyo. "NYC Parks inapinga vikali kuwekwa kwa vinyago visivyoidhinishwa katika bustani za jiji, bila kujali ukubwa wake," alisema msemaji wa Sam Biederman.Mabaki ya kinyago cha Donald Trump mjini New YorkMaafisa wa kampeni wa Donald Trump kufikia sasa hawajazungumzia vinyago hivyo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: