BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU AKATAA MADAWATI MABOVU NA KUPOKEA MADAWATI 14 TU KATI YA 102 YALIYOTOLEWA NA MENEJA MORO.

 
Mafundi wakitengeneza madawati eneo la Fire Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati, uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.

Waziri Mkuu aligomea madawati hayo jana wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi, ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS.

Alisema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati, lakini hawezi kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.

"Ofisa Elimu njoo, kagua haya madawati, yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya, huu si wakati wa kupokea vitu vibovu," alisema.

Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo, madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.

Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti na kuuagiza uongozi wa wilaya, ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa kuyakagua, kabla ya yeye kukabidhiwa.

Katika hatua nyingine, aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo, kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada, hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao," alisema.

Awali, Mbunge wa Mvomero, Suleiman Saddiq ‘Murad’ alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili wilaya hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba, hivyo alimuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.

Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima, Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi, watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa ; na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: