BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZAO LA NYANYA LAKOSA SOKO MOROGORO

 
Ashton Balaigwa 
HABARI ZA BIASHARA.
WAKULIMA wa nyanya wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamepata hasara kutokana na zao hilo kukosa soko na kupungua bei kutoka Sh. 20,000 hadi 2,000 kwa ndoo ya lita ishirini.

“Hivi sasa ndoo moja ya nyanya imeshuka kutoka Sh. 20,000 hadi 2,000, haijawahi kutokea na imetukatisha tamaa kuendelea na kilimo ambacho hakina tija,” alisema Mwenyekiti wa Wakulima wa Nyanya wa Kijiji cha Makuyu, wilayani humo, Mbaruk Seleman.

Kufuatia mkwamo huo, wakulima wa Kijiji cha Makuyu, wameiomba serikali kuwajengea viwanda vya kusindika nyanya ili waweze kuziongeza thamani na kujikwamua kiuchumi.

Maombi hayo ya ujenzi wa viwanda hivyo yamekuja kufuatia wakulima hao kupata hasara msimu wa mwaka huu kutokana na zao hilo kukosa soko na kulazimika kuuzwa kwa bei nafuu.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake, Mwenyekiti wa Wakulima wa Nyanya, Mbaruk Selemani, alisema ujenzi huo wa viwanda utawahakikishia soko la na usindikaji, ajira na biashara kwa kuuzwa katika maeneo ambayo hayana uzalishaji.

Alisema hata wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya kusindika nyanya waliokuwa wananunua zao hilo kwao, wameshindwa kununua kutokana na wengi kuwa na mashamba makubwa ya nyanya.

Josephine Mateke mkulima mwingine, alisema nyanya zinaozea shambani kutokana na kukosa soko la ndani na hata uwezekano wa kutafuta soko la nje haupo hivyo hushindwa kurudisha gharama walizotumia wakati wa maandalizi na uzalishaji.

Mateke aliiomba serikali kuwatafutia soko la nje ili kuuza zao hilo, pamoja na kuruhusu wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika viwanda vya usindikaji wa nyanya ili wakulima wapate sehemu ya kuuza. 


Hivi karibuni, Mkoa wa Morogoro ulisema unaendelea na mazungumzo na wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya matunda na mboga kwa kuwa mkoa huo umekuwa wazalishaji wakubwa huku kukiwa hakuna masoko.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: