BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZIARA YA WAZIRI MKUU SOKO LA MWANJELWA LAIBUA SIFA ZA PONGEZA MKUU WA MKOA KWA HATUA ALIZOCHUKUA ZA KUGUNDUA UFISADI UJENZI NA UPANGISHAJI WA SOKO

Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Aagiza Hatua Kali zichukuliwe watakaobainika ktk ripoti
Waziri Mkuu kassim Majaliwa leo amefanya ziara YA kustukiza soko la mwanjelwa na kumpongeza Mkuu Mkoa wa Mbeya kwa hatua alizochukua kwa kuunda Kamati YA uchunguzi kuhusiana na ujenzi wa siji hilo kujengwa kwa gharama kubwa ikilinganishwa na thamani halisi.


Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa Mkoa kupitia ripoti YA awali YA Kamati YA uchunguzi ikabidhiwe kwa CAG ili afanye ukaguzi kwa undani zaidi.

Ametoa muda wa siku Tatu Mkuu wa Mkoa aagize vyombo vya uchunguzi kubaini zilipo sh 489,000,0000 ambazo zilitolewa na CRDB lakini hazionekani zilipo.

Mkuu wa Mkoa ndiye aliyeibua ufisadi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa baada ya kubaini soko hilo kujengwa kwa shilingi bilioni 26 badala YA sh bilioni 16.


Aidha ni Mkuu wa Mkoa aliyeingilia kati kupunguza kodi ktk soko hilo jambo ambalo Waziri Mkuu amempongeza sana kwa ujasiri
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: